Harmonize aachana na meneja wake

0
177

Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize kutoka WCB aitwae Mr Puaz ameacha kazi ya kumsimamia mwanamuziki huyo kwasababu ya kutokuwa na maelewano.

Mr Pauz amefunguka na kusema kuwa ameamua kuacha kumsimamia mwanamuziki huyo baada ya kukosa maelewano siku za hivi karibuni.

Meneja huyo amesema kuwa kwasasa hafanyi kazi na Harmonize kwa sababu ya kupishana kauli lakini hawana bifu lolote kabisa.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa japokuwa ameacha kumsimamia mwanamuziki huyo lakini hana tofauti na lebo ya WCB na wataendelea kufanya kazi kama kawaida inapohitajika kwani hana tataizo nao.

Kwa upande wa Harmonize bado hajazungumza chochote kuhusu suala la meneja wake huyo kuacha kumsimamia kazi zake za kimuziki.

LEAVE A REPLY