Harmoize afunga mwaka na ‘Wapo’

0
25

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameachia wimbo mwingine kabla ya kumalizika kwa mwaka 2020 huku ikiwa tumebakiza siku 1 na masaa kadhaa kuumaliza mwaka amewaahidi mashabiki ifikapo saa 6 kamili usiku wa leo ndipo ataachia wimbo huo.

Wimbo wake huo mpya ameupa jina la Wapo ambapo kupitia post ya kava ya wimbo huo amendika ujumbe wa kuwatia nguvu wapambanaji wote kutokukata tamaa na kuamini hakuna atakaye waonea huruma na wala kutamani wao kupata mafanikio pamoja na furaha kwenye Maisha yao kikubwa ni kwa wao kuficha machozi yao.

Kupitia post yake harmonize ameandika haya “ONE MORE SONG 2020 🤔 OK..!! SPECIAL
MESEG TO YOU BROTHERS & SISTERS MPAMBANAJI MWENZANGU.

Pia ameendelea kuandika ULIOPO MTAAANI SIO KILA ANAEKUPIGIA MAKOFI ANAKUPONGEZA WAPO WANAO KUPIGIA ILI UMALIZE KUONGEA AMKA PAMBANA …!!!! DUNIA NDIVYO ILIVYO FICHA CHOZI LAKO UKILITOA HADHALANI  WAPO WANAOFURAHIA NA SIO KUKUONEA HURUMA KAMA UNAVYO DHANI.

LEAVE A REPLY