Hamisa Mobeto awajia juu wanaombeza kuzaa na Majay na Diamond

0
162

Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya kusema kuwa yeye sio Single mothers.

Siku ya juzi ilikuwa ni Mother’s Day/ siku ya Mama duniani na Hamisa aliweka wazi kuwa yeye sio Single mother kwa sababu anasaidiwa kulea watoto wake na Baba watoto wake.

Hamisa ana watoto wawili ambapo mtoto wake wa kwanza Fantansy amezaa na Majizzo na mtoto wake wa pili Dylan amezaaa na Diamond Platnumz.

Lakini baada ya video hiyo kuingia mtandaoni watu walianza kumsema vibaya kutokana na yeye kuongelea suala lake la kuzaa na wanaume wawili tofauti ambao wote ameweka wazi wana uwezo.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa altoa povu hili:

“Alafu ngoja niwaambie kitu. Mimi ni mbaya kweli nakubali kabisa, alafu pia ni maskini kweli kwenye maisha bado najikongoja kwahiyo hayo sio matusi bali ni hali halisi. Kwahiyo mkikubali hali kama niliyokubali mie labda mtaacha matusi yasio na faida.”

Aliongeza kuwa “Alafu miaka inaenda siku zinakimbia pia…hamuwezi kuwa mna hasira kila siku kisa nimezaa na wanaume wenye hela..hivi nachanganyikiwa au? maana sababu ningine hamna zaidi ya hao wanaume wawili.”

Aliendelea kuandika hivi, “Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga wazazi wa hawa watoto wawe nani.

LEAVE A REPLY