Hamis akanusha kutaka pesa kujiunga Konde Gang

0
23

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis ambaye amejulikana kupitia shindano la kusaka vipaji la BSS amekanusha kutaka pesa ili kujiunga na Konde Gang.

Taarifa za awali zilisema kuwa msanii alihitaji pesa nyingi ili kujiunga Konde Gang baada ya msanii Harmonize kuonyesha nia ya kutaka kumsaidia.

Hamis BSS amesema si kweli kwamba alihitaji pesa nyingi ili kujiunga Konde Gang, pia amefurahi kuona wasanii wengine walivyotambulishwa Konde Gang bila ya hata yeye kuwepo.

“Si kweli kwamba nilihitaji pesa nyingi  kujiunga na Konde Gang, ila ni riziki tu Mungu anatoa kwa kila mtu, mimi kiukweli nimefurahi kwa wasanii waliotambulishwa.

Pia amesema Naamini Mungu tu anafanikisha kwa kila mtu kwa wakati wake ila kwa kawaida natamani ningekuwa mimi”.

LEAVE A REPLY