Halmashauri nchini zapewa somo

0
78

Halmashauri nchini zimetakiwa kuweka mikakati madhubuti ya upatikanaji wa takwimu sahihi ili kusaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Benard Makali amesema hayo mjini hapa wakati wa ufunguzi wa warsha ya uhamasishaji wa malengo ya maendeleo endelevu kwa mikoa ya Manyara, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora.

wanarushiana mpira kwa kuwa hakuna kanzidata, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wasaidie katika hilo,” alisema.

Amesema malengo endelevu ya dunia ni muendelezo wa malengo ya milenia ya dunia (MDGs) ambayo muda wake ulimalizika mwaka 2015.

Ambapo serikali ilichukua hatua za kuruhusu wananchi kupaza sauti zao kuhusu mafanikio na matatizo ya utekelezaji wa malengo hayo.

Pia uandaaji wa mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano, 2016/2017 hadi 2020/2021 umezingatia malengo ya maendeleo endelevu na hivyo kurahisisha utekelezaji wa malengo hayo nchini katika ngazi zote.

Amesema malengo ya milenia ya dunia yaliainishwa katika malengo makuu manane, shabaha 18 na viashiria 18 na masuala mengi kwenye mpango huo yalihusisha kuondoa umaskini katika jamii katika maeneo ya elimu, usawa wa kijinsia na mazingira.

Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa mpango wa miaka mitano ambao unatafsiri azma ya Tanzania kuwa ya uchumi wa kati kwa kupitia mageuzi katika sekta ya viwanda. Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango, Servus Sagday alisema Tanzania imepiga hatua kubwa lakini umaskini wa kipato bado ni mkubwa.

LEAVE A REPLY