Hali ya Mwana FA yaimarika baada ya kukutwa na virusi vya Corona

0
331

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amewashukuru waliomtumia salam za pole na kuelezea hali yake ya kiafya inavyoendelea toka alipogundulika kuwa amepata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwana FA amendika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa “ Nawashukuru kwa salamu za pole na dua ndugu zangu. Kama nilivyosema,sijisikii kuumwa tena hata,KABISA.

Pia Ameendelea kusema kuwa Hata ile homa iliyonipa wasiwasi nikaenda kupima haijarudi toka jana.Malaria ina tabu zaidi ya kaugonjwa haka nawaambia. Asikutishe mtu.

Mwanamuziki huyo amejiangaza kuwa ni muhathirika wa ugonjwa huo baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona ambavyo vinaendelea kuenea kwa kasi dunia kote.

Mwanamuziki huyo ni mmoja wa waathirika wa ugonjwa huo nchini Tanzania na kufanya idadi kufikia watu 6 walioathirika na ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY