Hali ya Ally Choki yazidi kuimarika

0
56

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ally Choki amesema kuwa kwasasa hali yake ya kiafya inaendelea vizuri tofauti na zamani baada kutibiwa.

Ali Choki amedai kuwa kwasasa anafurahi baada ya hali ya afya yake kuzidi kuimarika baada ya kuugua ghafla mwezi uliopita na kusababisha hali ya taharuki kwa baadhi ya mashabiki wake nchini.

Choki amesema kuwa kwasasa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hivyo Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu ataendelea na kazi ya muziki katika bendi anayoitumikia kwa sasa ya Super Kamanyola jijini Mwanza.

Ally Choki amesema kuwa “Hali yangu inaimarika kila siku, Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu nitapanda jukwaani kama kawaida kwa ajili ya kuwapagawisha mashabiki wangu,”.

Mwanamuziki huyo kwasasa amehamishia makazi yake jijini Mwanza ambapo anafanya kazi chini ya bendi ya Super Kamanyola.

LEAVE A REPLY