H Baba akanusha kuachana na mkewe Flora Mvungi

0
289

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamisi Ramadhan maarufu kama H Baba amekanusha kuachana na mkewe Flora Mvungi licha ya mwanamke huyo kukiri kuvunjika kwa ndoa hiyo.

H Baba amesema kwamba kitu anachojua ni kwamba Flora bado ni mkewe kwani yeye ndiye aliyeoa, hivyo kama ni talaka yeye ndiye mwenye kuitoa lakini kamwe hajafanya hivyo.

H Baba ameendelea kusema kwamba kauli ya Flora kuwa ndoa ya wawili hao imekufa sio kweli, na kama Flora ndiye aliyeoa basi atoe talaka ili kuvunja ndoa hiyo.

“Maisha yangu ya muziki hayaingiliani na familia yangu na watoto, sikumuoa instagram, kwa sababu unapozungumza ili watu wakusikie, ili u-trend sio kitu cha busara kwa sababu unaongea uongo, mimi ninachojiua ni mtu ambaye sijampa talaka, na mtu ambaye hatuna ugomvi, mimi niko busy na baishara zangu”.

 

Taarifa ambayo imetolewa na mwenyewe Flora Mvungi kuwa wawili hao wameachana jambo ambalo H Baba amelipinga vikali.

LEAVE A REPLY