Gwajima amewatembelea Clouds Media na kuwapa pole

0
324

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo ametembelea ofisi za Clouds Media zilizopo Mikocheni B kwa ajili ya kuwapa pole kutokana na tukio la kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askali wenye silaha.

Gwajima amewasili katika ofisi za Media hiyo mida ya saa nne asubuhi akiwa na msafara wa magari manne akiwa na ulinzi wa hali juu.

Alipowasili mchungaji huyo alipokelewa na mkurugenzi wa vipinidi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba pamoja na vingozi wengine wa Media hiyo.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari, Gwajima amesema kuwa amesikitishwa sana na hatua iliyochukuliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ya kuvamia ofisi hizo akiwa na askari polisi wenye silaha.

Gwajima amesema kuwa hana nia mbaya na Clouds kutokana na yaliyotokea kwasababu watangazaji waliotaka kuripoti tukio lake walikuwa wamefosiwa na mkuu wa mkoa kufanya hivyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mtahaba amemshukuru Gwajima kwa kuwatembelea ofisi kwao na kuwapa pole kwa yaliyowafika mwishoni mwa wiki.

LEAVE A REPLY