Gurdiola kushtakiwa na FA

0
169
Pepe Gurdiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameshitakiwa na Chama cha Soka nchini England kwa kuvaa nguo yenye ‘Ribbon’ ya njano inayodaiwa kubeba ujumbe wa kisiasa kitu ambacho hakiruhusiwi michezoni.

Guardiola alionekana amevaa fulana hiyo kwenye mchezo wa FA ambapo timu yake ya Manchester City iliondolewa na timu ya Wigan Athletic ambapo FA imedai kuwa ni kinyume na sheria za soka.

Guardiola anadaiwa kuvaa hivyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono harakati za wananchi wa Catalan ambao wanapigania kujitenga na serikali ya Madrid. Guardiola ni mzaliwa wa Santpedor huko Catalonia Hispania.

Sio mara ya kwanza kwa Gaurdiola kuvaa hivyo ambapo pia mwezi Novemba mwaka jana kwenye moja ya mechi za ligi alivaa na akapewa onyo. Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amepewa muda hadi Machi 5 awe amewasilisha utetezi wake.

Guardiola anatarajiwa kuiongoza Manchester City kwenye mchezo wa fainali yake ya kwanza tangu aanze kukinoa kikosi hicho atakapokabiriana na Arsenal, ikiwa ni fainali ya kombe la ligi.

LEAVE A REPLY