Gugu Zulu afariki dunia akipanda mlima Kilimanjaro

0
299

Dereva wa wa mbio za magari mwenye mafanikio kutoka Afrika Kusini, Gugulethu Zulu a.k.a ‘The fastest brother in Africa’ amefariki dunia leo hii wakati akipanda mlima Kilimanjaro kwaajili ya kukusanya fedha za kusaidia mfuko wa taasisi ya Nelson Mandela.

Inadaiwa kuwa Gugu alipata matatizo ya kupumua na kikosi cha uokoaji kilimuwekea dripu kabla ya kuteremka nae kutoka Mlimani.

Gugu alikuwa njiani kuelekea kileleni ambapo wenzake wanatarajia kufika leo.

Dereva huyo aliwahi kutuma picha akiwa njiani kwenye mlima huo akiwa na mkewe kwenye siku ya pili na siku ya tatu huku akionekana kufurahia safari hiyo na pia kukiri kusumbuliwa na ugonjwa wa mafua.

Zulu alianza kazi ya udereva wa bio za magari mwaka 1999 baada ya kuhitimu kwenye chi cha Isondo Racing Academy na kisha kushinda mashindano mbalimbali ikiwemo Vodacom Isondo Sports 2000 national championship.

Majonzi: Marehemu Gugu Zulu enzi za uhai wake akiwa na familia yake
Majonzi: Marehemu Gugu Zulu enzi za uhai wake akiwa na familia yake

LEAVE A REPLY