Gigy Money amjia juu shabiki yake

0
60

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amemjia juu shabiki wake baada ya kuhoji ukimya wake kwenye muziki.

Msanii huyo aliwataka mashabiki wake wamuulize maswali akiwa hewani (live) na ndipo shabiki huyo alipomuuliza ‘kazi mpya lini.

“Nahitaji muda wa kupumzika, watu wamenijua kabla ya kuanza kujiingiza kwenye muziki, kwa nini kuulizauliza hivi. Ndiyo maana Vanessa Mdee aliwahi kusema ‘muziki ni kitu ambacho kinachoweza kukufanya uishi maisha ya shida sana’,” alisema Gigy.

Gigy aliendelea kumjia juu shabiki huyo anaodai kuwa yeye hatoi nyimbo, akiwasihi wamuache aishi anavyotaka na mtoto wake na siyo kuulizwa maswali kama hayo.

LEAVE A REPLY