Gigy Money akitamani kifo

0
215

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money ameeleza kwamba anatamani kufariki Dunia, kwa sababu anaona hawezi kula wala hawezi kulala.

Kupitia post aliyoweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram Gigy Money amesema, hawezi kuamini kinachomtokea, anaona anajichukia mwenyewe na amekuwa dhaifu.

“Natamani kufariki bila sababu yoyote, siwezi kula wala siwezi kulala kwa kifupi siamini na hii imezidi, sasa najichukia mimi mwenyewe na nimekuwa dhaifu, yaani inauma ila inabidi uwe mkubwa kuelewa, sipo “interested” na mtu yeyote yule wote wamenishinda nimechoka” ameandika Gigy Money.

Gigy Money ameonesha kuyalalamikia mapenzi, hii imekuja baada ya kupita siku mbili tangu kugombana na mpenzi wake raia wa Nigeria Hunchy Huncho, ambaye alimfukuza nyumbani kwake.

LEAVE A REPLY