Gigy Money ajuta kutaja orodha ya wanaume aliotoka nao kimapenzi

0
1151

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’ amesema kuwa anajuta kutaja hadharani orodha ya wanaume aliotoka nao kimapenzi.

Gigy Money amekiri anajutia kutaja orodha hiyo ya wanaume kwani mpaka leo kuna wanaume wanaogopa kumtongoza kwa kuogopa kuanikwa.

“Kuwataja wanaume nilipitaga nao najutiaga sana, inafanya kuna muda nikose vitu vya maana kwa kuogopa kuwa nitaropoka.

Amesema kuwa “Kumbe ule ni utoto na ni foolish age kila mtu lazima apitie hata uikimbie ni bora uipitie ukubwani usiirudie. Kwahiyo najutia kuwataja wanaume niliowahi kutembea nao ila sijutii kupitia ile hatua,“.

Mwaka jana Gigy Money alitaja wanaume zaidi ya 10 wengi wakiwa mastaa wa muziki wa Bongo Fleva na watangazaji wa Redio na TV.

LEAVE A REPLY