Gazeti la Daily Mail la Uingereza lakubali kumlipa mke wa Trump

0
147

Gazeti la Uingereza la Daily Mail limekubali kumlipa mke wa rais wa Marekani, Melania Trump baada ya kuchapisha habari ya kumkashifu.

Gazeti hilo lilikuwa limeandika kuwa Melania Trump wakati mmoja alifaya kazi kama kahaba kipindi cha nyuma.

Taarifa hiyo ilichapjshwa wakati wa kampeni nchini Marekani ambapo Trump ameshinda uchaguzi huo.

Melania Trump alikubali msamaha kutoka kwa gazeti hilo kwenye mahakama mjini London ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa.

Mke huyo wa Rais wa Marekani alipeleka kesi mahakamani mwezi Februari mwaka huu akitaka kulipwa dola milioni 150 za Marekani.

Melania Trump alisajiliwa na shirika moja la mitindo akiwa bado msichana na kuanza kusafiri kote Ulaya na Marekani na kushiriki katika warsha kubwa.

Alikutana na Donald Trump mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka 28 kwenye sherehe wakati wa wiki ya mitindo mjini New York nchini Marekani na wakafunga ndoa miaka saba baadaye.

 

LEAVE A REPLY