Gavana Pence kuwa mgombea mwenza wa Trump?

0
91
Mwenza?: Donald Trump akiwa na Gavana wa jimbo la Indiana, Mike Pence

Tetesi za uteuzi wa mgombea mwenza wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican zimeanza kuenea huku gavana wa jimbo la Indiana, Mike Pence akitajwa kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi mkuu.

Donald Trump Addresses GOP Lincoln Day Event In Michigan

Iwapo gavana Pence atathibitishwa na Donald Trump, anatarajia kuwa makamu wa rais wa Marekani iwapo chama cha Republican kitashinda uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, Trump akiwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News amedai kuwa bado hajafanya uamuzi wake wa mwisho kabisa.

Wajumbe wa kampeni wa Trump walitarajia kumtangaza rasmi mgombea mwenza siku ya leo ingawa wameahirisha tukio hilo kutokana tukio la ugaidi lililoua watu 84 nchini Ufaransa.

Gavana Pence anaaminika kuwa na ushawishi mkubwa kwa wanachama wakubwa wa chama cha Republican.

LEAVE A REPLY