Gauni la harusi ya Lulu gharama yake ni hatari

0
81

Gauni la harusi alilolivaa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akifunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu, Francis Ciza ‘Majizo’ limegharimu Sh25 milioni.

Gauni hilo limebuniwa na mbunifu wa mavazi aliyewabunia watu maarufu nchini Marekani kama Beyonce na Card B.

Kwa mujibu wa moja ya wabunifu wa mavazi walioshughulikia gauni la Lulu, Kenneth Shirima maarufu Kenny The Brand amesema gauni hilo la mtindo wa Cinderella limebuniwa na mbunifu kutoka nchini Kosovo anayetwa Valdrin Sahiti.

“Limebuniwa na Sahiti, lilivyokuja hapa (Tanzania) mimi nimelifanyia kitu kinachoitwa fitting (kurekebisha limtoshe Lulu),” alisema Kenny.

Mwaka 2019 Sahiti alimtengenezea gauni rapa kutoka Marekani, Card B ambalo alilivaa kwenye tangazo la mji wa Las Vegas, na mwaka jana staa maarufu wa muziki duniani, Beyonce alivaa gauni ambalo pia lilitengenezwa na Sahiti.

LEAVE A REPLY