Gabon yampa mikoba Jose Antonio Camacho, siku 43 kabla ya AFCON

0
102

Timu ya taifa ya Gabon imemteua kocha wa zamani wa Real Madrid, Sevilla, Espanyol, Benfica na timu ya taif aya Hispania Jose Antonio Camacho kuwa kocha mkuu wa wenyeji hao wa kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Camacho mwenye miaka 61 anakabiliwa na kibarua kigumu kwani ana siku 43 pekee za kukiandaa kikosi hicho na michauno ya AFCON inayotarajiwa kuanza mwezi Januari mwakani.

Kabla ya uteuzi huo, Camacho alikuwa nje ya soka kufuatia kuota nyasi kwa kibarua chake cha kukinoa kikosi cha China mwaka 2013.

Camacho amepewa mkataba wa miaka miwili kufuatia kutimuliwa kazi kwa mtangulizi wake, Jorge Costa aliyetimuliwa mwezi uliopita.

Camacho, mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taif aya Hispania atakuwa na kibarua cha kwanza cha mashindano atakapoishuhudia timu yake ikicheza na Guinea Bissau mwenye mechi ya ufunguzi wa AFCON.

Pia Camacho anatarajiwa kukiongoz kikosi hicho kutafuta nafasi ya kufuzu kwa kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

LEAVE A REPLY