Gabo na Wema wazindua filamu yao mpya ‘Kisogo’

0
314

Waigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba na Wema Sepetu wamezindua filamu mpya yao mpya iitwayo ‘Kisogo’.

Filamu hiyo itaonekana na mtu yeyote mwenye simu ya mkononi ya kisasa (smartphone) kupitia application iitwayo Uhondo.

Wakizungumza kwenye uzinduzi wa filamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam waandaaji wa filamu hiyo Kampuni ya Sarafu Media inayomilikiwa na Gabo Zigamba, wamesema filamu hiyo ipo tofauti na filamu nyingi zilizozoeleka Bongo na hata namna ya kupatikana kwake kwa urahisi.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, mtumiaji wa simu akishadownload  app ya Uhondo anaiona kwenye orodha ya filamu zilizopo ambapo itakuwa na dakika thelathini.

Kampuni hiyo wamesema kuwa dakika kumi na tano za kwanza zitatolewa bure ili kila mtu ajionee ambapo sehemu ya pili yenye dakika kumi na tano pia, itauzwa kwa shilingi mia tano tu.

Kwa upande wake  Gabo alisema haikuwa kazi nyepesi kukamilisha filamu hiyo, hasa katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa kwamba Bongo Movie hazina ubora.

 

LEAVE A REPLY