Gabo, muigizaji anayependa kusoma vitabu

0
45
Gabo

Muigizaji wa Bongo Movie, Salim Ahmed almaarufu kama Gabo Zigamba amefunguka na kusema kuwa yeye ni mtu anayependa sana kusoma vitabu.

Gabo amesema kuwa anapenda kusoma sana vitabu vya Shaaban Robert, kwa wiki anaweza akaenda maktaba hata mara mbili au tatu.

Amesema kuwa “Sehemu yangu pendwa sana ninayopenda kwenda kutuliza akili ni Maktaba ya Taifa, pale ndipo utanikuta nasoma sana vitabu vya Shaaban Robert.

Pia amesema kuwa Kwanza ni skills kuwa poa, la pili kuendelea kusoma kadiri unavyozidi kuishi, kwa hiyo mimi nimekuwa nikisoma vitabu mbalimbali hii inanifanya kuandika mambo yanayoeleweka mtandaoni,”.

Gabo ni muigizaji wa Bongo Movie anayefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo Movie kutokana na ubora wa uigizaji katika movie.

LEAVE A REPLY