Gabo awajia mashabiki wa filamu za Bongo

0
31
Gabo

Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amefunguka kuhusu tabia ya watu kufananisha tasnia ya filamu za kibongo na marehemu Steven Kanumba.

Gabo amesema kuwa watu kufananisha tasnia na uwezo wa marehemu ni kosa kwa sababu ya ubora wa tasnia hiyo.

“Tasnia ni kubwa sana ikifananishwa na marehemu Kanumba watu watakuwa wanakosea kwa sababu  issue iliyokuwepo ni uchache wa kazi kuweza kuonekana, lakini kingine ni sehemu za kuweza kutolea kazi, usambazaji na content zimekuwa ni shida sana”

Aidha amenyoosha maelezo kuhusu kinachoikwamisha tasnia ya filamu hapa nchini kwa kusema “ Dharau ndiyo kitu kikubwa kinachoumiza katika tasnia ya filamu, ni mfumo wa machungu unaotengeneza chuki katika tasnia ya filamu zetu.

 Pia amesema kuwa maisha yangu na maisha ya Industry ni vitu viwili tofauti, naishi katika watu wawili ambao wanamjua Gabo kupitia filamu waendelee kumjua hivyo wakinijua maisha yangu nje ya tasnia itakuwa matusi kwangu”.

LEAVE A REPLY