Gabo anavyowachukia watu wanafiki

0
11
Gabo

Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amefunguka na kusema kuwa kwenye maisha yake hapendi kabisa marafiki ambao wanafiki.

 

Gabo amesema kuwa aina hiyo ya watu ni vigumu sana kuishi nao lakini pia kuna muda mwingine hauwezi kuishi bila wao.

 

Muigizaji huyo amesema kuwa kwenye haya maisha hakuna watu wabaya kama wanafiki, furaha yao ni kuchonganisha watu tu na siyo kitu kingine.

 

Pia Gabo amesema kuwa watu wanafki huwa ni ngumu sana kuishi nao lakini pia kuna muda mwingine hauwezi kuishi bila wao maana kuna wakati wanakuletea habari ambazo zinasaidia,”.

 

Muigizaji huyo kwasasa anafanya vizuri kwenye soka la uigizaji kutokana na ubora wa uigizaji wake kwenye movie na tamthilia mbali mbali.

LEAVE A REPLY