Gabo aibuka baada ya kuzushiwa kifo mtandaoni

0
68
Gabo

Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa na tabia ya baadhi ya watu mitandaoni kuzusha vifo kwa wenzao kupitia mitandao hiyo.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kuzushiwa kifo katika katika mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo la kweli kwani yeye ni mzima wa afya kabisa.

Gabo aliweka screenshot ya taarifa ya uzushi uliodai kuwa alifariki kwa ajali akikanusha na kuelekeza jicho kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania kuwashughulikia watu hao.

Gabo ameonesha kuumizwa na ushuzi wa taarifa hizo dhidi yake, aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa analiacha katika mikono ya imani tu.

LEAVE A REPLY