Gabo afunga ndoa

0
70

Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba, amefafanua sababu za kufunga ndoa ya siri kwa kusema mambo ya kuoa ni vitu binafsi vya mtu.

Taarifa za msanii huyo wa filamu kuoa zilikuja baada kusambaa kwa picha mitandaoni, siku ya Aprili 21, zikimuonesha katika mavazi na mazingira ya harusi yaliyoashiria kwamba anafunga ndoa.

Gabo Zigamba ameeleza kuwa, “Huwa sipendi kuzungumzia hivyo vitu kwa sababu kuna vitu viwili, kwanza mtu anayeniona anatafuta uhamasishaji kutoka kwangu,sasa kuhusu ndoa siwezi kumhimiza mtu na haifanani kabisa sawa na duka la vipodozi kwenda kuulizia sigara”.

“Pili Suala la mimi kuoa au kutokuoa kwa mtu ambaye anamfuatilia Gabo Zigamba haimsaidii chochote, kuoa, kuolewa au kufanya maulid  haina uzito wowote kwa jamii.

Pia amesema kuwa hayo ni mambo ya mtu binafsi japo Ulaya wanafanya sana hizo Style kwa sisi bado hasa ukiangalia soko letu halipo rasmi, kuna vitu vingi vya kupiga kelele ili tuweze kusogea”.

LEAVE A REPLY