Fred Uisso aipaisha Tanzania kwenye mashindano ya upishi duniani

0
323

Mtaalamu wa mapishi kutoka nchini Tanzania, Fred Uisso ambaye alikuwa anashiriki mashindano ya dunia ya upishi nchini Marekani ameibuka kidedea na kuiwakilisha vyema Tanzania baada ya kunyakua nafasi ya nne kwenye mashindano hayo.

Uisso ambaye kabla ya kushinda nafasi hiyo alishaweka historia ya kuwa mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kushiriki kwenye shindano hilo aliwabwaga wapishi wengine 21 kwenye mchuano ulioshirikisha wapishi 25 kutoka hoteli kubwa na maarufu duniani.

Uisso aliyetangazwa na mkurugenzi wa World Food Championship, Mc Cloud alfajiri ya leo ni mpishi mkubwa hapa nchini na ubora wa mapishi yake umemfanya apewe mikataba ya kutangaza bidhaa mbalimbali za vyakula.

Picha kwa hisani: RedGold

LEAVE A REPLY