Francis Cheka ageukia upromota wa ngumi

0
157

Bingwa wa zamani wa mchezo wa ndondi kwa mikanda ya WBC na WBO, Francis Cheka amefungua kampuni yake ya kuandaa na kusimamia mapambano mbalimbali ya ndondi ikiwemo kumsimamia yeye mwenyewe kwenye mapambano yake.

Kampuni hiyo inayoitwa Cheka Promotion imeshakamilisha usajili wake wa kisheria na inatarajia kuandaa pambano lake la kwanza baina ya bondia wa Tanzania Cosmas Cheka ambaye anatarajia kupambana dhidi ya bondia kutoka Uganda mwezi Disemba mwaka huu.

Bondia huyo amesema pia ameamua kufungua kampuni hiyo ili kukuza vipaji vya mabondia chipukizi pamoja na kukuza mchezo wa ndondi nchini.

LEAVE A REPLY