Foodles Production yashtakiwa kwa kusababisha Harrison Ford kuvunjika mguu

0
190

Kampuni ya filamu ya Foodles Production (UK) Ltd ambayo inatengeneza filamu maarufu za ‘Star Wars’ imekubali makosa mawili mahakamani baada ya muigizaji mkongwe Harrison Ford kuvunjika mguu akiwa kwenye mazoezi ya kutengeneza filamu hiyo.

Harrison Ford mwenye umri wa miaka 74 alivunjika mguu baada ya kuangukiwa na mlango kwenye jukwaa la Pinewood kwenye ukumbi wa Millenium Falcon Juni 2014.

Foodles Production (UK) Ltd inayomilikiwa na kampuni ya Disney ilishtakiwa kwa makosa manne kwenye mahakama ya Milton Keynes.

Hukumu kamili ya kesi hiyo itatolewa Agosti 22 baada ya mahakama hiyo kuyafuta mashtaka mawili kati ya hayo manne.

LEAVE A REPLY