Flora Mbasha amjibu Emmanuel Mbasha kuhusu kunyimwa mtoto

0
245

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amefunguka juu ya kitendo cha aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha kumlalamikia kumnyima mtoto.

Flora ambaye kwasasa anafahamika kama Madam Flora amesema kuwa kitendo alichofanya Emmanuel Mbasha si kizuri kwasababu ameongelea suala hilo kupitia mitandao ya kijamii wakati suala hilo liliongelewa mahakamani.

Wiki iliyopita Emmanuel Mbasha alitumia akaunti yake ya Instagram kumlaumu mumewe huyo kutokana kumyima kumuona mtoto wake aliyezaa na Flora jambo ambalo linamnyima raha.

Flora Mbasha amesema hawezi kulizungumzia suala la hilo kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao, kwani yeye ndio anaujua ukweli, na iwapo mahakama ilimpa haki ya kumuona mtoto, kuandika kwenye instagram sio sahihi kwani mahakama haipo instagram.

Wawili hao walitalikiana baada ya kesi aliyokuwa akituhumiwa Emmanuel kuisha na kukutwa hana hatia, na kisha Flora kuolewa na mwanaume mwengine.

LEAVE A REPLY