Fid Q anapomfundisha Q Chillah ‘Elimu asiyoijua’ kwa njia ya ‘asiyoitarajia’

0
1224

Kila mfuatiliaji wa muziki hapa nchini atakuwa anajua kuwa Ngosha Ze Don ni Fid Q na ndiye huyo huyo Farid Kubanda na wakati huo huo kila mmoja akijua kuwa Shaaban Katwila ndiye Q Chillah.

Sababu za kuwajua hawa ni namna walivyofanikiwa kuwateka wapenzi wa muziki hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla licha ya kuwa muziki wanaoimba ni tofauti na kuwa hata ‘MITAZAMO YAO HAIFANANI KABISA’.

Mwaka jana, Q Chillah alinukuliwa akijiita ‘Mungu wa Bongo Fleva’ huku mwaka huu Fid Q akimwambia shabiki wake ambaye alidiriki kumuita ‘Mungu wa Hip Hop’ kuwa asimuite tena jina hilo.

Utakachogundua hapa ni kuwa kuna wasanii ‘wanajikweza lakini wanaenda mbali sana hadi kukufuru na kuna wasanii wanakwenza na watu hadi kufikia hatua ya mashabiki hao kukufuru na kutaka kuwakufurisha wasanii hao’.

Tofauti ya wasanii hawa ni kukosa mitazamo au maneno muafaka ya kujielezea au kueleza matakwa yao huku wengine wakiwa na hekima kubwa ya kuepuka yale wanayotambua kuwa ‘sio hadhi yao’.

Q Chillah anapoamua kujiita Mungu ‘Unapata jibu kuwa kauli hii ni LAANA na ndio maana KAZI ZAKE HAZIFANYI VIZURI’.

Fid Q, Big up!! kwa ‘kuuona mtego wa anguko lako na kuukwepa’!!

fid-q

LEAVE A REPLY