Fid Q afunguka waliokimbia na michango ya msiba wa Godzilla

0
116

Mwanamuziki wa hip hop bongo, Fid Q amewaweka wazi watu waliokimbia na pesa za michango ya rambi rambi kwenye msiba wa msanii Godzilla aliefariki wiki iliyopita.

Fid Q amesema kwamba wachangishaji walikuwa wengi, lakini baadhi ya michango ilifika ikiwemo iliyokusanywa na Niki Mbishi, Soggy Dogy na Wakazi.

Baadhi ya wachangishaji kwenye vidaftari kuna baadhi hawakufikisha kabisa pesa hizo za rambi rambi.

Kutokana na hayo Fid Q amesema watu hao bado wana nafasi ya kuzirudisha na kuwasilisha kwa familia ya Godzilla lakini wasipofanya hivyo Mungu ndiye atawahukumu.

Tasnia ya Bongo Fleva ilipatwa na msiba wa msanii mwenzao Godzilla, ambaye alifariki Februari 13 baada ya kuugua ghafla.

LEAVE A REPLY