Fid Q afunguka sababu ya kumposti mpenzi wake mtandaoni

0
149

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Fid Q amefunguka sababu ya kuposti picha ya mpenzi wake mtandaoni.

Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake  ya kijamii ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu.

Amesema kuwa ”Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza ndoa”.

Kwa upande wake mrembo huyo wa Fid Q amesema hawashangai sana wanawake wanaomtongoza Fid kwenye ‘Social network’ kwa kuwa mpenzi wake anamuonekano mzuri na ni mwanaume ambaye ameshapitia mambo mengi duniani hivyo anaamini kwamba atakuwa mwanaume bora kwake.

LEAVE A REPLY