Fid Q afunguka sababu ya kifo cha Pancho

0
145

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Fid Q ameweka wazi kuwa baada ya kupata taarifa za kifo Pancho alikwenda kuungana na watu waliokuwa na Pancho kwaajili ya taratibu zaidi.

Fid Q amesema kuwa ni kweli Pancho amefariki kwa ajali ya maji na kifo chochote cha ajali kinakuwa kinahusisha polisi kwahiyo wameripoti kituo cha Polisi Kawe kwaajili ya kupata kibali na tayari mwili umehifadhiwa Mochwari ya Lugalo.

Fid Q amefafanua kuwa Pancho amefariki dunia leo jioni kwa kuzama baharini akiwa katika kisiwa cha Mbudya Dar es salaam hivyo kwa kuwa wameshatoa taarifa polisi taratibu zingine zitaendelea.

Amesema baada ya kumaliza taratibu za kuweka mwili Mochwari usiku huu, wanafanya taratibu za kukutana na familia yake ili kupanga zaidi kwaajili ya mazishi na ratiba zingine hivyo kufikia kesho wataeleza ratiba kamili.

Pancho amefanya kazi mbalimbali katika studio tofauti huku akidumu zaidi B-Hitz, ambako alitengeneza ngoma kama Dar es salaam Stand up ya Chid Benz, Bye bye Joh Makini, Ndege mtini Ferooz.

LEAVE A REPLY