Fid Q afunga ndoa jijini Dar

0
87

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo , Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi katika Msikiti wa Qiblatain Boko Jijini Dar es Salaam.

Fid Q hakutoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo lakini wasanii wenzake ambao walihudhuria tukio hilo wamempongeza kwa hatua hiyo kubwa.

AY ambaye alihudhuria ndoa hiyo alipost picha na kumpongeza rapa huyo kwa hatua hiyo kubwa katika maisha yake.

“Hongera sana ndugu yangu @therealfidq kwa kufunga ndoa Inshaalah Mwenyezi Mungu Aibariki Ndoa Yenu.

Naye meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amempongeza rapa huyo na kuandika “Ongera Mtani @therealfidq na karibu kundini Mungu awasimamie kuilinda ndoa yenu maana kwenye imani ya dini yetu hapa umepanda daraja.

LEAVE A REPLY