Fayvanny awashangaa wanaobeza kazi yake ya mavazi

0
35

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aitwae Fayvanny amesema kuwa, watu wanaochukia kazi zake za mavazi kipindi hiki, ipo siku watamkubali tu.

Fayvanny amesema siku zote ili ufanikiwe, lazima utakutana na vikwazo vya kila aina, hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu na ndiyo maana alivyoshambuliwa mitandaoni kuhusu mavazi yake, hakujali.

Nashangaa baadhi ya watu wanavyosema kuwa mimi sina damu ya kupendwa, binafsi sijali kuhusu hilo kwa sababu akinipenda Mungu pekee inatosha.

Pia mwanadada amesema kuwa ridhiki anatoa Mungu na sio wao, nawaona jinsi wanavyoponda kazi zangu, lakini niwaambie tu kwamba, huu ni mwanzo bado vitu vizuri vinazidi kuja.

LEAVE A REPLY