Familia ya Q Chilla yaingilia kati mkataba wake na QS Mhonda

0
242

Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva kuingia mkataba na meneja anayefahamika kwa jina la QS Mhonda familia ya mwanamuziki huyo imengilia kati na kutaka kuvunjwa kwa mkataba huo.

Familia ya Q Chilla imeamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo ya kifamilia.

Baba mdogo wa Q Chila amesema kwamba hofu juu ya mkataba ni kwamba haukuwa na ushahidi wowote kwa upande wa Q Chilla hali inayombana na kushindwa kuendelea kimaisha na kushindwa kuwa na  nyumba yake.

Baba mdogo huyo ameendelea kusema kuwa familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chillah ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.

Familia hiyo imeamua kuingilia kati mgogoro wa mkataba huo kutokana na mkataba huo kutokidhi vigezo kutokana na kukosa ushaidi upande wa Q Chilla.

LEAVE A REPLY