Faiza Ally azua zogo uwanja wa ndege

0
56

Msanii wa Bongo Movie, Faiza Ally alizua fujo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Fujo hizo zilijiri baada ya kutukanwa na askari mmoja kwa kua­mbiwa anajiuza kisa kikiwa ni dira alilokuwa amevaa ambalo lilimuonyesha nguo ya ndani.

Faiza alisema hakuna siku ambayo aliumia kama hiyo kwa sababu kwanza alivaa nguo aliyoamini ni ya heshima na hakujua kama ilikuwa inaonesha nguo ya ndani.

“Niliumia sana na kuamua kufanya timbwili zito kwa kugombana na yule askari kwa sababu alinitukana bila sababu, huwezi kwenda kumpokea baba watoto wako halafu mtu aseme unajiu­za, ku­vaa vile ilitokea bahati mbaya wala sikudhamiria kwani nilitoka haraka haraka kumuwahi mgeni,” alisema Faiza.

Aidha Faiza alidai kuwa alilazimika kwenda kushtaki kwenye uongozi wa uwanja huo lakini nako alikutana na utara­tibu ambao ulimkatisha tamaa na kuamua kuachana na kesi hiyo.

LEAVE A REPLY