Ewura yatangaza bei mpya ya petroli

0
98

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kushuka kwa nishati ya mafuta aina ya petroli kwa mwezi Agosti.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zinazoanza kutumika leo zimeshukwa kwa Sh36 na Sh44 kwa lita ya petrol na dizeli.

Taarifa hiyo inasema kwamba tofauti ni katika mafuta ya taa ambapo bei yake imeongezeka kwa Sh24 kwa lita, hali iliyosababishwa na kuongezeka kwa gharama ya usafirishaji wa bidhaa katika mfumo wa Uagizwaji wa Mafuta kwa Pamoja (BPS).

Wastani wa matumizi ya mafuta kwa siku ni lita milioni tano kwa mafuta ya dizeli, Lita milioni tatu kwa mafuta ya Petrol na Lita 100,000 kwa mafuta ya taa.

Kutokana na bei hizo mpya, kuanzia leo lita moja ya petrol katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,978 kutoka ilivyokua mwezi uliopita ya Sh2,014, wakati lita ya dizeli sasa itauzwa Sh1,830 kutoka Sh1,874 na mafuta ya taa yatapanda mpaka Sh1,830 kutoka Sh1,806 kwa lita kwa mwezi uliopita.

Mhandisi Samweli amesema kwa Mkoa wa Tanga, hakutakuwa na mabadiliko kwa petroli na dizeli kwa sababu hakuna mzigo uliopokelewa kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi wa saba 2017.

LEAVE A REPLY