EVE akutana na baba yake baada ya miaka 25

0
212

Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, EVE amekutana na baba yake mzazi baada ya kumtelekeza miaka 25 iliyopita.

EVE amesema kuwa baada ya kukutana na kuongea nae sasa anafikiria kumsamehe kwa kitendo alichofanya cha kumtelekeza wakati akiwa mtoto.

Baba yake alimwacha EVE akiwa na umri wa miaka 12 na kuja kumuona tena akiwa na miaka 37.

Eve amesema baada ya kuongea na Baba yake ameelewa kwanini alikimbia familia wakati akiwa mtoto mdogo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa baba yake wakati anamzaa alikuwa na umri mdogo na kushindwa kumudu malezi yake pamoja na mama yake kwani kipindi hiko anazaliwa mama yake alikuwa ana umri wa miaka 17.

EVE amesema kuwa ameanza kufikiria kumsamehe baba yake baada ya kumtekeleza miaka 27 iliyopita kutokana alifanya kosa hilo pasipo matarajio yake.

LEAVE A REPLY