EU yamteua Michel Barnier ‘kumalizana na Brexit’

0
141
Umoja wa Ulaya umemchagua waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa, Michel Barnier  kuwa msimamizi mkuu wa majadiliano ya kujiondoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya, maarufu kama Brexit.
Tangazo la uteuzi huo limetolewa na rais wa tume ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker amesema kazi hiyo inahitaji alimuhitaji mwanasiasa mwenye uzoefu kwaajili ya kazi hiyo ngumu.
Bwana Barnier ambaye aliwahi kushika wadhifa wa ukuu wa tume ya EU, anakumbukwa sana kwa mapinduzi yake ya kibenki ambayo hata hivyo si maarufu sana nchini Uingereza.
Kupitia ujumbe wa akaunti ya Twitter, Bw. Barnier amesema ametukuzwa kupewa nafasi hiyo hivyo anashukuru.
Bwana Barnier anatarajiwa kufanya kazi na mwakilishi wa Uingereza kwenye majadiliano hayo, David Davis ambaye alikuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za kuitaka Uingereza ijitoe EU.
Majadiliano yataanza mara tu Uingereza itakapoitekeleza kanuni ya kifungu cha 50 cha katiba ya EU.

LEAVE A REPLY