Ethiopia yaondoa majeshi yake nchini Somalia

0
169

Ethiopia imeondoa majeshi yake katika mji muhimu katikati mwa Somalia.

Dhusamareb sasa unadhibitiwa na wapiganji walio na msimamo wa kadri, wa Ahlu Sunna Waljama’a.

Kundi la Ahlu Sunna limekuwa likikabiliana na kundi la al-Shabab ambalo linadhibiti maeneo mengi ya Somalia.

Wachanganuzi wanasema Ethiopia inaondoa vikosi vyake kutokana na ukosefu wa uungwaji mkono na jamii ya kimataifa.

Al Shabab linamiliki miji mingi iliowachwa na vikosi hivyo vya Ethiopia.

Ethiopia huchangia vikosi vya Umoja wa Afrika lakini pia ina wanajeshi wengine nchini Somalia.

LEAVE A REPLY