Ethiopia: Wafungwa washtakiwa kwa kuchoma moto gereza, kuua wenzao

0
177

Mahakama ya Ethiopia imewafungulia mashtaka mapya wafungwa 38 kwa kosa la kula njama, kushambulia, kuua na kuchoma moto gereza mwezi Septemba.

Wafungwa hao wanadaiwa kufanya uhalifu huo wakati wa tukio la kuungua kwa gereza la Kilinto ambapo zaidi ya wafungwa 20 walipoteza maisha.

Mashtaka hayo yamekuja kufuatia kupingwa vikali kwa ripoti ya awali iliyotolewa na serikali na kudai kuwa wafungwa hao walikufa kwa kukosa hewa.

Wanaharakati mbalimbali nchini humo walidai kuwa miili ya wafungwa hao ilikutwa na matundu ya risasi pamoja na michubuko iliyoashiria mateso na mauaji ya kukusudia.

Hata hivyo sasa Serikali imekuja na ripoti inayodai wafungwa waliouawa walilazimishwa kujiunga na makundi yaliyopigwa marufuku nchini humo na walipokataa walipigwa na walichomwa moto siku ambayo gereza hilo liliunguzwa.

LEAVE A REPLY