Espanyol yavunja rekodi ya Real Madrid

0
167

Klabu ya soka ya Real Madrid jana imefungwa 1-0 dhidi ya Espanyol kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uhispania.

Kabla ya mchezo huo Real Madrid ilikuwa ikishikilia rekodi ya kutofungwa na Espanyol kwa zaidi ya miaka 10, rekodi ambayo imevunjwa na bao la dakika ya 90+3 la mshambuliaji Gerard Moreno.

Baada ya kuanza msimu vibaya, Real Madrid ilikuwa imeanza kurejesha makali yake baada ya kushinda mechi tano mfululizo, lakini jana ikiwa bila ya nyota wake Cristiano Ronaldo ikakubali kichapo hicho.

Espanyol ilikuwa haijashinda hata mchezo mmoja katika michezo yake  22 iliyopita dhidi ya Real Madrid huku ikitoa sare mechi tatu tu tangu Oktoba 2007. Mechi ya jana ilikuwa ni mechi ya 23 katika kipindi cha miaka hiyo.

Real Madrid sasa imesalia katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 51 kwenye mechi 26 ikiwa nyuma kwa alama 14 dhidi ya vinara FC Barcelona wenye alama 65.

LEAVE A REPLY