Eric Aniva ‘Fisi’ afungwa miaka miwili jela na ‘kazi ngumu’

0
237
In this photo taken Thursday, June 30, 2016, Eric Aniva is photographed near Blantyre, Malawi. Malawian police on Tuesday July 26, 2016 have arrested Aniva who said he was hired by families to have sex with more than 100 young women, including children, in what was described as ritual cleansing. The country's president ordered the man's arrest after he told international media about his actions and said he is HIV-positive. (AP Photo/Eldson Chagara)

Raia wa Malawi aliyepata umaarufu mkubwa siku za karibuni baada ya kufanyiwa mahojiano na shirika la BBC na kukiri kutembea na wajane wapya na wasichana zaidi ya 100 huku akijitambua kuwa ni muathirika wa VVU amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na kazi ngumu.

Eric Aniva maarufu zaidi kama ‘Fisi’ amepata adhabu hiyo kwa kufanya mapenzi na wajane na wasichana hao bila kutumia kinga huku akifahamu hatari ya kuwaambukiza VVU.

Vitendo hivyo vya ngono alivyokuwa kivifanya ni sehemu ya utamaduni wa baadhi ya makabila ya nchi hiyo ambapo familia za wanawake wanaofiwa na waume zao au zile zenye mabinti wanawari huwapeleka kwa ‘fisi’ kwaajili ya kufanya mapenzi ikiwa ni ishara ya kuondoa mikosi ya kimapenzi kwa waathirika wa vitendo hivyo.

Rais wa Malawi Peter Mutharika aliagiza kukamatwa kwa Aniva na kushtakiwa lakini waathirika wa vitendo vyake hawakujitokeza kutoa ushahidi mahakamani.

Hivyo, Aniva alishtakiwa kwa kosa la kufanya mila yenye madhara kwa jamii ambapo mahakama imemkuta na hatia na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela.

LEAVE A REPLY