Enock Bella alia na menejimenti mbovu

0
494

Mwanamuziki wa Bongo Fleva aliyekuwa memba wa Yamoto Band, Enock Bella amesema kuwa sababu inayofanya nyimbo zake kutofika mbali ni kukosa menejimenti ya uhakika ya kusimamia kazi zake.

Bella amesema kuwa nyimbo zake hazifanyai vizuri kwasababu hana menejimenti ya uhakika kama walivyo wasanii wenzake Aslay, Mbosso na Beka Flavour ambao walikuwa wote Yamoto Band.

Kauli ya muimbaji huyo inakuja mara baada ya kuachana na menejimeti iliyokuwa inamsimamia kutoka nchini Uganda kutokana na kutofikia makubaliano.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ameshafanya kazi nyingi lakini hadi sasa hakuna ngoma ambayo imemuweka kwenye ramani kutokana na menejimenti yake kushindwa kuzipushi ngoma hizo ili zifanye vizuri.

Eneck Bella amefanya vibao kama Sauda, Ngoja Kidogo, Nitazoea pamoja na mpya inayoitwa Kurumbembe ambayo kwasasa inafanya vizuri.

LEAVE A REPLY