Enock Bella afunguka sababu ya kutojiunga WCB

0
316

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Enock Bella amefunguka na kusema kuwa wakati Yamoto Band inavunjika alitamani kujiunga na lebo ya WCB chini ya Diamond Platnumz.

Mmoja ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Yamoto Bendi, Enock Bella amesema wakati kundi hilo lilipo vunjika alitamani kujiunga na lebo ya WCB, Lebo ambayo ilimchukua na kumsimamia msanii Mbosso ambaye pia alikuwa kwenye kundi hilo.

Enock Bella amesema wakati hana menejimenti ya kusimamia kazi zake alitamani kuwa sehemu ya WCB ili muziki wake uweze kufika mbali kama vile alivyokuwa anataka.

Bella amesema alienda mbali zaidi nakuamua kuzungumza na viongozi wa WCB ili waweze kumpa nafasi lakini ilishindikana.

‘’Tulishawahi kuongea nakumbuka kitu cha mwisho walichonambia, alisema bela usichoke usidhani unachokifanya hakina msingi wala watu hawakioni.

Pia amesema kuwa tunadhamini uwezo wako tutajua namna ya kukusapoti, tukisema tukuchukue huwezi jua watu wanaweza sema Diamond ndo sababu ya Yamoto kuvunjika au labda mkubwa kuna kitu alikifanya labda Enock na Mboso wachukuliwe alafu wale wengine wapalanganyike kila mtu aende kivyake.

LEAVE A REPLY