Enock Bella afunguka kuhusu Yamoto Band

0
403

Aliyekuwa mwanamuziki wa kundi la Yamoto Band, Enock Bella amesema kuwa mashabiki wao wasitegemee kuona wanafanya kazi pamoja kama hapo awali.

Enock Bella amefunguka kuwa pamoja na watu wengi kudai kuwa bendi hiyo imekufa lakini yeye hana taarifa hizo bali anachojua kuwa wamepeana nafasi ili kila msanii aweze kufanya kazi kivyake.

Enock Bella ambaye kwa sasa anafanya muziki wake kama msanii wa kujitegemea ameweka wazi kuwa kwa sasa kundi hilo kurudi kama zamani itakuwa ngumu.

Bella ameendelea kusema kuwa kama ikitokeaa kufanya kazi ya mara moja basi watafanya makubaliano fulani ila kwa sasa kila msanii anafanya vizuri mwenyewe;

Enock Bella nae ametoa wimbo mpya akiwa peke yake baada ya wasanii wenzake Aslay na Beka Flavour kutoa nyimbo zao kitambo.

LEAVE A REPLY