Edu Boy afunguka kumchana Fid Q kwenye wimbo wake Tunasafisha

0
191

Mkali wa hip hop Bongo kutokea pande za Mwanza, Edu Boy amefunguka na kusema kuwa wasanii wanamchukulia Fid Q kama mtu asiyekosolewa lakini kwa upande wake yeye anamchana kama kawaida.

Kupitia wimbo wake mpya ‘Tunasafisha’ Edu Boy amemchana Fid Q kwenye mstari uliosema kuwa ‘Game noma mpaka Fid ame-shake, ashukuru remix isingekuwa fresh’.

Msanii huyo amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakimuogopa Fid Q kumchana lakini yeye ameeleza kile ambacho amekiona katika ngoma ya Fresh ila si kwa ubaya.

Edu Boy ni msanii anayesikfika kwa kuwachana wasanii wenzie kuhusu maisha yao ndani ya muziki wa hip hop pamoja na Bongo Fleva.

LEAVE A REPLY