Ebitoke ang’atuka Timamu

0
306

Mchekeshaji maarufu Bongo, Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke ametangaza kujiondoa kwenye kundi lake la Timamu Africa alilokuwa akifanya nalo kazi zake za sanaa.

Ebitoke amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameeleza kwamba hatua hiyo imekuja kufuatia mkataba wake na Timamu kumalizika, hivyo ameamua kuondoka ili akafanye kazi sehemu nyingine.

“Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, kuanzia sasa nitakua nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV, nikimaanisha mkataba wangu umeisha,” ameeleza Ebitoke.

Mbali na kufanya kazi ya uchekeshaji, mwaka huu Ebitoke amecheza filamu yake ya kwanza tangu aanze kuigiza inayoitwa Sema ambayo uzinduzi wake wa awali ulifanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Aidha, ndani ya TIMAMU, Ebitoke alikuwa akishirikiana na wachekeshaji wengine kama Bwana Mjeshi Mr. Beneficial na Mama Ashura ambaye kitambo hajaonekana na Mkali Wao ambaye alishahama kitambo.

LEAVE A REPLY