Duma afunguka sababu ya kumleta msanii kutoka Australia

0
212

Muigizaji wa Bongo Movie, Daudi Michael ‘Duma’ amesema lengo kumuita nchini msanii kutoka nchi ya Australia John K ni kutaka kuirudisha hadhi ya filamu ambayo imepotea kwa kipindi kirefu.

Duma amesema kuwa baada ya kumpokea mgeni wake huyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

 “Watanzania wanapaswa watupe ushirikiano sana katika kazi zetu, nimemleta John K ili niweze kuridisha heshima ya filamu nchini nchini Tanzania na kuonesha jinsi gani Duma anavyopanda kwaajili ya ‘industry’ nasio kwa mtu mmoja mmoja”.

Pamoja na hayo, Duma ameendelea kwa kusema “sina matatizo na mtu yeyote, lakini naona hii hatua ya kumuita John K tutafika tunapotaka kwasababu John K muda huu Australia na nje ya Australia anafanya vizuri sana”.

LEAVE A REPLY