Dully Sykes kuanzisha lebo ya muziki

0
29

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes ametangaza ujio wa lebo yake ya muziki itakayoitwa ‘Misifaz Music’ ambayo itakuwa inasaidia wasanii kutoka kimuziki.

Dully Sykes ametangaza neema kwa wasanii wa muziki ambao walikuwa na matamanio ya kuongozwa na kusimamiwa kimuziki na mwanamuziki huyo mkongwe aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na nyimbo zake.

Dully ametangaza ujio wa record label yake mpya ya Misifaz muziki ambayo kwa sasa yupo yeye mwenyewe hivyo amewataka wasanii wengine waungane nao kwenye lebo hiyo.

Dully amesema kuwa nia ya kuanzisha lebo hiyo ni kuwasaidia wasanii wachanga ambao hawajatoka kimuziki hivyo anataka kuwasaidia kwa kuwatambulisha kwa watanzania.

Msanii huyo siyo wa kwanza kuwa msanii anayemiliki record label kwa sasa ambapo kwa sasa kun label kama WCB, KONDE MUSIC WORLD WIDE, KINGS MUSIC, MDEE MUSIC na THE INDUSTRY.

LEAVE A REPLY